Alhamisi, 9 Julai 2015

Wajue waimbaji nguli wa Injili Africa Mashariki

Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili Rose Muhando akiwa jukwaani akitumbuiza mkoani Iriga.
Na Elisha Magolanga

KAMA utahitajika kuwataja wasanii wanawake kumi wanaofanya vizuri katika muziki wa Injili Bongo na hata Afrika Mashariki, haitakuwa rahisi kuyaacha majina ya Rose Mhando, Bahati Bukuku, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Christina Shusho, Siana Ulomi, Martha Mwaipaja, Jeni Miso na Jennifer Mgendi.

Hii ni kwasababu ndiyo wanaongoza kwa usambazaji na soko la nyimbo za injili ambazo huwezi kipita maduka mawili ya CD ukakosa kazi zao.

Katika wakati ambao wanamuziki wa Bongo Flava na dansi wanalilia kupata soko la kazi zao, waimbaji wa Injili wanaendelea kula kuku kwa mrija kwani kazi zao sokoni zinanunuliwa kama njugu.

Kwa baadhi ya nchi, nyimbo zao hupigwa hata katika kumbi za starehe kwa kuamini ni nyimbo za kujirusha kutokana na mvuto wake.

Rose Mhando

Huyu ndiye kiboko yao, wanamuziki wa Bongo Flava wanamfahamu kwa jinsi anavyowapiga bao katika uuzaji wa kazi zake, si tu katika CD na video, Rose Mhando pia ni kinara wa mauzo katika miito ya simu.

Diamond ambaye anasifika kwa kuuza miito ya simu, akikutana na Rose Mhando anakaa chini kwani mapema mwaka huu alimwacha mbali kwa kuingiza Sh29 milioni ndani ya miezi mitatu huku Diamond akiingiza Sh21 milioni.

Albamu zake za ‘Mteule Uwe Macho’, ‘Kitimutimu’, ‘Jipange Sawasawa’, ‘Utamu wa Yesu’, na 'Facebook' bado zinaendelea kufanya vizuri pamoja na kuwa wasanii wengine wanaingiza albamu mpya kila kukicha.

Bahati Bukuku

Huyu anatajwa kushikilia nafasi ya pili ya mauzo ya CD na video katika maduka mbalimbali ya kazi za sanaa Bongo. Pamoja na kutotoa kazi mpya mara kwa mara, albamu yake moja ilimfanya kuwa mwimbaji namba mbili katika mauzo na matamasha nchini.

Tamasha lolote la Injili haliwezi kukamilika bila kupigwa nyimbo kama ‘Waraka wa Amani’, ‘Nimesamehewa Dhambi’, ‘Nyakati za Mwisho’ na ‘Mapito’.

Mwanamuziki huyu kwa sasa anatamba na albamu iitwayo ‘Dunia Haina Huruma’.

Upendo Kilahiro

Inavyoonekana muziki wa Injili unamlipa sana kwani ameweza kuanzisha Chuo cha Ushonaji kiitwacho, New Day Africa Foundation, ambacho wanafunzi wake hawalipi hata shilingi moja kwa muda wanaochukua ujuzi chuoni hapo.

Kilahiro anayetamba na nyimbo za 'Ni nani kama wewe', ‘Unajibu Maombi’, ‘Usinipite’, na 'Zindoga na Ziwelale', ni msanii mwanamke namba tatu kwa mauzo ya nyimbo za Injili Bongo.






Upendo Kilahilo

Upendo Nkone


‘Niacheni Niimbe’, ‘Nimebaki na Yesu’, ‘Uniongoze Yesu’ na ‘Nakaza Mwendo’, ni baadhi ya nyimbo zinazofanya kazi zake ziendelee kununuliwa kwa wingi. Kila anapoachia wimbo mpya, huendelea kuzifanya zile za zamani ziwe nzuri zaidi.

Mbali na kuuza kazi zake, pia ni mwanamuziki anayeongoza kwa kufanya matamasha ndani na nje ya Bongo. Mara kwa mara hufanya ziara nchini Marekani kwa mwaliko wa kaka yake Mchungaji Donis Nkone na Kenya ambako anakubalika na kuheshimika sana.





 Upendo Nkone 

Christina Shusho

Huyu anazo sababu zaidi ya mia moja za kuwa mwanamuziki anayeuza sana katika muziki wa Injili. Kwanza sura yake inapokaa kwenye ‘kava’ inampa mteja hamu ya kutoa pesa yake kununua CD, pili unapopata bahati ya kuisikia sauti yake kwa mara ya kwanza, hakika utataka kuisikia tena na tena na tatu tungo zake zinazogusa maisha ya kawaida na kiroho zimekuwa kivutio kikubwa. 


Msanii huyu kwa sasa anatamba na Albam yeke mpya 'Umenifanya Ning'are' na ndiye msanii anayeongoza nyimbo zake kuchezwa redioni 

Christina Shuso

Flora Mbasha, Jeni Misso, Jennifer Mgendi, Martha Mwaipaja na Siana Olomi nao wanaingia kwenye kundi hilo, lakini wanapishana kidogo kutokana na sababu mbalimbali zilizotolewa na wafanyabiashara wa kazi hizi.

Waimbaji Jeni Misso, Martha Mwaipaja na Siana Olomi ni kama wanachipukia kwenye soko kuu la kazi hizi, lakini wamekuwa wakichuana na wakongwe akina Flora Mbasha na Jennifer Mgendi ambao wamekuwa katika muziki huu kwa muda mrefu.

Wafanyabiashara wa kazi hizi wanasema, Jennifer Mgendi na Flora Mbasha, waliwahi kuwa vinara wa mauzo lakini walipoanza kujichanganya na biashara nyingine iliwapunguzia mashabiki ambao walianza kununua kazi za waimbaji wengine.

Flora Mbasha kujihusisha na kampeni mbalimbali zikiwamo za vyama vya siasa na Jennifer Mgendi kujiingiza katika uigizaji wa filamu, zinatajwa kuwa ni sababu zilizowarudisha nyuma.

Yote kwa yote hii ndiyo ‘krimu’ ya wasanii wanaoongoza sokoni kwa muziki huo, tamasha lolote la muziki wa Injili Bongo au Afrika Mashariki, haliwezi kukamilika bila uwepo wa waimbaji hawa.

Kwetu pazuri yarekodi Santuri muonekano ya 12

Kwaya ya Christian Ambassador kutoka nchini Rwanda wakirekod DVD yao toleo la 12 hivi karibuni (Picha na Warren  na Mutabazi) 

Na Roland Robert

Kundi maarufu la kwaya ya Kisabato kutoka nchini Rwanda, Ambassadors of Christ limerekodi santuri muonekano (DVD) mpya, katika tukio lililofanyika katika viwanja vya chuo kikuu cha Kisabato tawi la Gishushu nchini humo.


Kwamujibu wa blog ya Mtangazaji Maduhu inasema lengo la kurekodi toleo hilo la 12 lenye nyimbo za Kinyarwanda ni kutangaza injili na kuwaunganisha wanyarwanda baada ya mauaji ya kimbali ya mwaka 1994.

Katika rekodi hiyo pia waimbaji waliowahi kuvuma na kwaya hiyo kama solo wao mwanadada Mbabazi Milly Kamugisha alikuwa mmoja wa waimbaji waliorekodi na kwaya yake hiyo baada ya kutubu kisha kurejeshwa kundini miezi kadhaa iliyopita.

Bila kumsahau shemeji na wifi wa Watanzania mwanadada mwenye sauti nzuri ya kwanza aliyeolewa na Mtanzania aitwaye Claire Warren na ambaye makazi yake kwasasa yapo nchini lakini pia alijumuika na wenzake katika tukio hilo 

Ambassadors wakiwa jukwaani tayari kwa zoezi la kurekodi DVD

Faith Choir and Praise Team Baada ya ibada







Alhamisi, 25 Juni 2015

Ukitaka kuwa mtunzi mzuri wa Nyimbo za Injili zingatia...


Mwana Muziki wa injili,  John Mtangoo pia ni mwalimu wa Kwaya ya Tumaini Arusha maarufu Shangilieni



Na John Mtangoo

Njia bora ya kutunga wimbo wa Injili


1. Mjue na umpende Mungu Jehova.

2. Imba kwa ajili ya nafsi yako na mahusiano yako na Mungu kama ni kwa ajili ya wimbo wa sifa ama kuabudu. Kama ni wimbo wa uinjilisti angalia mazingira yanayokuzunguka na hapo utapata ujumbe wa kutungia wimbo.
3.Wimbo wako ubebe sifa zote kwa Mungu na usitake wewe ndiye ubebe hizo sifa. Weka malengo ya Mungu kuinuliwa kwanza.

4. Usilenge kufaidika na utunzi wako muache Mungu afaidike na uandishi wako ndipo yeye ataamua akufanyie nini.Kumbuka baraka za Mungu zinautoshelevu kuliko za kibinadamu.

5. Tafuta msaada kwa mtu mwenye uelewa zaidi wa mziki anaweza kukuongezea maarifa ya utunzi.

Mambo usiyotakiwa kufanya katika kutunga wimbo.

6. Usitunge wimbo wa matukio ya mda mfupi kama nia ni wimbo udumu. Unaweza tu kutunga wimbo maalum kwa tukio maalum.Kwa mfano kuna siku kuu fulani inaendana na wimbo fulani hiyo haina shida.

7. Usitunge wimbo ili wewe uwe maarufu wala usitake maoni ya watu juu ya wimbo uliotunga. wewe tunga kama nafsi inavyokuongoza.


8. Usitunge wimbo unaofanana na wafulani kwa sababu fulani amefanikiwa. Ni vema kusimama kwa miguu yako ila unaweza mtembelea huyo aliyefanikiwa ili mshirikishane maarifa.

Jambo la Msingi na kukumbuka mara zote ASIYEJUA HUWA HAPOTEI NJIA NA SIKU ZOTE WANAOJUA HUWA HAWAJUI KAMA WANAJUA BALI WASIOJUA HUAMINI WANAJUA. Waandishi bora wa nyimbo ni marafiki sana na Tabia za unyenyekevu. Nyenyekea chini ya mkono hodari wa Mungu iliakukweze kwa wakati.

Tujikumbushe tulikotoka

Aliyekuwa M/Kiti wa Faith Choir, Joshua Mwasandube akicheza kiduku siku ya sherehe ya kuwaaga  wahitimu



Aliyekuwa Mwalimu wa Faith Choir 2012/2013 Emmanuel Mchomvu akikabidhiwa cheti siku ya kuwaaga wahitimu




Upendo Mandara akifurahia kupokea zawadi siku ya sherehe ya kuwaaga waimbaji wahitimu

Faith kwaya wakiimba katika ibada