Alhamisi, 25 Juni 2015

Ukitaka kuwa mtunzi mzuri wa Nyimbo za Injili zingatia...


Mwana Muziki wa injili,  John Mtangoo pia ni mwalimu wa Kwaya ya Tumaini Arusha maarufu Shangilieni



Na John Mtangoo

Njia bora ya kutunga wimbo wa Injili


1. Mjue na umpende Mungu Jehova.

2. Imba kwa ajili ya nafsi yako na mahusiano yako na Mungu kama ni kwa ajili ya wimbo wa sifa ama kuabudu. Kama ni wimbo wa uinjilisti angalia mazingira yanayokuzunguka na hapo utapata ujumbe wa kutungia wimbo.
3.Wimbo wako ubebe sifa zote kwa Mungu na usitake wewe ndiye ubebe hizo sifa. Weka malengo ya Mungu kuinuliwa kwanza.

4. Usilenge kufaidika na utunzi wako muache Mungu afaidike na uandishi wako ndipo yeye ataamua akufanyie nini.Kumbuka baraka za Mungu zinautoshelevu kuliko za kibinadamu.

5. Tafuta msaada kwa mtu mwenye uelewa zaidi wa mziki anaweza kukuongezea maarifa ya utunzi.

Mambo usiyotakiwa kufanya katika kutunga wimbo.

6. Usitunge wimbo wa matukio ya mda mfupi kama nia ni wimbo udumu. Unaweza tu kutunga wimbo maalum kwa tukio maalum.Kwa mfano kuna siku kuu fulani inaendana na wimbo fulani hiyo haina shida.

7. Usitunge wimbo ili wewe uwe maarufu wala usitake maoni ya watu juu ya wimbo uliotunga. wewe tunga kama nafsi inavyokuongoza.


8. Usitunge wimbo unaofanana na wafulani kwa sababu fulani amefanikiwa. Ni vema kusimama kwa miguu yako ila unaweza mtembelea huyo aliyefanikiwa ili mshirikishane maarifa.

Jambo la Msingi na kukumbuka mara zote ASIYEJUA HUWA HAPOTEI NJIA NA SIKU ZOTE WANAOJUA HUWA HAWAJUI KAMA WANAJUA BALI WASIOJUA HUAMINI WANAJUA. Waandishi bora wa nyimbo ni marafiki sana na Tabia za unyenyekevu. Nyenyekea chini ya mkono hodari wa Mungu iliakukweze kwa wakati.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni