Faith Song Name: Niongoze Safarini: Key E
Composer: Elisha Magolana (20011)
1. Niongoze safrini Bwana unitangulie
Nisilemewe na dhambi mpaka mwisho wa safari x2
Duniani
kuna giza – Kubwa siwezi kuona
Jua nalo
limekuchwa – Limetoweka na nuru x2
2. Nimekuchagua wewe kaa ndani yangu mimi
Na maneno yako Bwana yaniongoze safari x2
Uniongoze
Bwana usinitelekeze
Neno lako
likawe nuru ya miguu yangu
Daima
niwe na wewe Bwana wangu
Katika
mikono yako sitaogopa lolote x2
Na-a-ku-tegemea
Bwana wangu Yesu
Nimeyakabidhi
maisha mikononi mwako
Hushindwi
kitu Bwana, hushindwi jambo lolote
Sina hofu
ninalindwa na jemedari wangu x2
Daima- Nasonga mbele, nasonga mbele, nasonga
mbele, sitaogopa
Nasema- Sirudi nyuma, sirudi nyuma, sirudi nyuma maana
niko nawe x2
Faith Song Name: Maisha Haya: Key D
Composer: Elisha Magolana (20014)
1. Maisha haya ndugu yangu duniani ni ya muda kitambo tuu-
Tunapita
Hebu safisha njia zako uwe safi siku
mauti ikifika wewe- U tayari x2
Karibu
Bwana ingia ndani yangu,
Safisha
sasa maisha yangu eee
Kwa kuwa
mimi sijui siku yangu
Ya kufa
hivyo nitakase Bwana x2
2. Siku za mwanadamu hapa duniani zimejaa shida na taabu-Tunaona
Tusiwe na huzuni sana yatupasa tumshukuru Mungu yeye-Muumba wetu x2
Najua
ndugu zangu wataomboleza
Siku ya
kufa kwangu mwenzangu
Wakizunguka
kuaga mwili wangu
Kama ni
safi ni Paradiso tuu x2
Hei heeee niokoe Bwana aah - usiniache nipotee dhambini
Hei heeee nirehemu Bwana aah- usiniache na mizigo ya
dhambi
Yahweee nisafishe Bwana aah- usiniache na uovu wangu
Yahweee niongoze Bwana aah- usiniache kati ya maadui x2
Faith Song Name: Bwana Ulinichagua: Key D
Composer: Elisha Magolana (20014)
1. Bwana ulinichagua mimi, ili- nikutumi-kie wewe
Nakumbuka
nyakati zile, nakumbuka pendo lako
Nili-asi
wi-to wako Bwana, Kwa ku-penda mambo ya dunia
Najutia
zamani zile, najutia uamuzi wangu x2
Ee
Bwana Yesu narudi nipokee mwanao
Dunia
imenisonga sina pa kutokea x2
Wewe
msaada wangu, tena kimbilio langu x2
Utukuzwe
Mungu juu mbinguni, usifiwe kwa upendo wako x2
Wewe
ndiwe dhamana ya maisha yangu naja kwako kwa uzuri Bwana aaah Umenipa
urithi kwa waokovu wako, naahidi kuwa nawe Bwana aaah x2
Bwana Mungu hapendezwi kuwaona wanadamu wakipote
Kamtuma
Yesu Kristo kuja hapa dunia kutuokoax2
Nakumbuka nyakati zile, nakumbuka pendo lako
Bwana Mungu hapendezwi kuwaona wanadamu wakipote
Kamtuma Yesu Kristo kuja hapa dunia kutuokoax2
Jipeleleze,
Matendo yako.........Oooh
Mwenendo wako,
Maisha yako x2
Faith Song Name: Tembea na Yesu: Key D
Composer: Elisha Magolana (20014)
Ulimwenguni
tunayo vita kuubwa na ya kutisha mwovu shetani ameivuruga dunia,
Si kwa
watoto, si kwa vijana hata watu wazima Ibirisi amewachakaza kabisa x2.
Dunia ni shida inanuka dhambi sasa Aah, hata utu wetu umezidiwa na wanyama,
Yasikitisha
sana ndoa za jinsia moja Aah, zinaingia makanisani kubarikiwa x2
Mwenzangu
amani ya kweli yapatikana yapatikana kwa Yesu
Mwenzangu
furaha ya kweli yapatikana yapatikana kwa Yesu x2
Oh! Tembea ah - Na Yesu
Safiri - Na Yesu
Oh! Tembea ah - Na Yesu
Safiri - Na Yesu
Kazini -
Na Yesu,
Sokoni -
Na Yesu x2
Popote
tembea na Yesu, siku zote tembea na Yesu
Masomoni
tembea na Yesu, usimwache tembea na Yesu x2
Rafiki
yangu mmoja wa karibu Eeeh alipotajirika akamwacha Yesu
Nilipomuuliza
alijibu Eeeh kwamba huko kwa Yesu hakuna starehe x2
Laiti angejua
kwa Yesu kwa Yesu iko furaha ya milele x2.
Oo!
Tenda Bwana - Tenda kitu
Kwa
makutano - Tenda kitu
Ili watu -wakuone wewe - Tenda Bwana
x2
Faith Song Name: Nimekukimbilia wewe: Key F
Composer: Elisha Magolana (20015)
Nimekukimbilia wewe- Mungu
wangu okoa maisha yangu naye mwovu.
Nimekutumaini wewe- Nisi-aibike
adui wasifurahi kunisinda x 2
Nakimbilia kwako Ee
baba
Niepushe na mabaya ya dunia
Bila masaada wako nitashindwa
Baba ninakuomba uniponye x2
Chunga sasa maisha yangu-
Niokoe wateesi wanifuata uniponye.
Uniongoze katika haki-
Nifundishe mapito yako baba unirehemu x2
Inapendeza ndugu yangu, kumpokea huyu Yesu
Ayatawale maisha yako, Atasamehe dhambi zako x2
Faith Song Name: Wavuvi: Key D
Composer: Elisha Magolana (20015)
Bwana Yesu alikuwa akipita
kando
Kando ya ziwa Galilaya
akihubiri
Akawaona wavuvi Simoni na
Andrea
Wakivua samaki kwa nyavu
zao x2.
Ndipo Yesu akawaambia,
nifuateni mimi nitawabadilisha
Nanyi mtakuwa wavuvi wa watu, na kuware-je-sha wale waliopotea x2.
Wakaondoka kumfuata Bwana Yesu
Waliziacha nyavu zao kwa haraka
Fundisho kwetu tusikiapo sauti
Tumfuate Yesu na kuacha dhambi zetu x2
Ni Yesu pekee anaweza
kukusamehe - Na kukubadilisha
Ni Yesu pekee ndiye jibu
la matatizo -Hebu mwite leo.... yako x2
Song Name : Ebenezer
By Angela ChibalonzaUmbali tumetoka, na mahali tumefika (This far we have come from, and where we are now)
Ndio maana ninatambua, kwamba wewe ni ebeneza (It is why I confess, that you are Ebenezer)
Sio kwa uwezo wangu,ila ni kwa uwezo wako (It is not because of my might, but by yours)
Mahali nimefika, acha nikushukuru (Thus far I have reached, let me thank you)
EE Bwana umenisaidia, nifike mahali nimefika (Oh Lord you have helped me, to reach where I am)
Bwana wewe ni ebeneza, maishani mwangu oo (Lord you are the Ebenezer in my life)
Ninataka Ebeneza, nijenge juu yako (I want to build on you Ebenezer)
Ninataka Ebeneza, uwe msingi yangu (I want you Ebenezer to be my foundation)
Jiwe langu la pembeni, nakutamani sana (My cornerstone, I desire you so much)
Jiwe langu la thamani, nakuhitaji sana (My valuable rock, I need you so much)
Oo Ebeneza, jiwe langu (Oh Ebenezer, my rock)
Ninataka maisha yangu, yajengwe juu yako (I want my life, to be founded on you)
NInataka ndoa yangu, ijengwe juu yako baba (I want my marriage, to be founded on you)
Ndoa zilizojengwa juu yako yahwe, hazivunjiki kamwe (because marriages built on you, can never be broken)
Nyumba zilizojengwa juu yako yahweh hazivunjiki kamwe (Homes founded on you Yahweh, can never be broken)
Ninataka uimbaji wangu baba, ujengwe juu yako (I want my singing Father, to be founded on you)
Maana wewe ni sauti yangu, wewe ni uzima wangu (For you are my voice, you are my life)
Ninataka Ebeneza, nijenge juu yako (I want to build on you Ebenezer)
Ninataka Ebeneza, uwe msingi yangu (I want you Ebenezer to be my foundation)
Jiwe langu la pembeni, nakutamani sana (My cornerstone, I desire you so much)
Jiwe langu la thamani, nakuhitaji sana (My valuable rock, I need you so much)
Oo Ebeneza, jiwe langu (Oh Ebenezer, my rock)
Ebeneza lang’a, libanga nangai ya tala
Ole kidya mape wolo papa ee kati na bomoyi nanga
Nzambe na kumisio, mokote ko nani nayo
Bisika nako milele o yahwe, ezali sela makasi nayo
Ninataka Ebeneza, nijenge juu yako (I want to build on you Ebenezer)
Ninataka Ebeneza, uwe msingi yangu (I want you Ebenezer to be my foundation)
Jiwe langu la pembeni, nakutamani sana (My cornerstone, I desire you so much)
Jiwe langu la thamani, nakuhitaji sana (My valuable rock, I need you so much)
Oo Ebeneza, jiwe langu (Oh Ebenezer, my rock)
Ebenezer ni jiwe langu, jiwe langu la msingi (Ebenezer is my rock, my cornerstone)
Mahali nimefika leo, Ni kwa ajili yako ebeneza (Thus far I have come, is because of you Ebenezer)
Mawe mengi yako hapa chini ya jua (There are a lot of rocks under the sun)
kuna dhahabu, kuna almasi Kuna mawe hata sijui majina yake (There is gold, there is diamond, and others I can’t name)
Lakini hakutawahi kuwa jiwe kama ebeneza (But there will never be a rock like Ebenezer)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni